Jeremiah 30:10-11


10 a“ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,
usifadhaike, ee Israeli,’
asema Bwana.
‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali,
wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.
Yakobo atakuwa tena na amani na usalama,
wala hakuna atakayemtia hofu.
11 bMimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’
asema Bwana.
‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote
ambamo miongoni mwao nimewatawanya,
sitawaangamiza ninyi kabisa.
Nitawaadhibu, lakini kwa haki.
Sitawaacha kabisa bila adhabu.’
Copyright information for SwhNEN